Urusi yaionya Magharibi kuhusu silaha za Ukraine
20 Septemba 2024Matangazo
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Urusi, Maria Zakharova, amewaambia waandishi wa habari kwamba mpango wa amani uliopendekezwa na Rais Volodymyr Zelenskiy wa Ukraine haukidhi vigezo vya kusuluhisha mzozo huo.
Soma zaidi: Rais Vladimir Putin asema wako tayari kwa mazungumzo na Ukraine, kwa kuzingatia makubaliano ya awali
Siku ya Jumatano (Septemba 18) Zelenskiy alisema Ukraine imekamilisha maandalizi ya mpango wa kuishinda Urusi ambao anakusudia kuujadili na Rais Joe Biden atakafanya ziara nchini Marekani wiki ijayo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergei Ryabkov, amesisitiza hii leo kuwa Marekani inapaswa kuzingatia onyo la Moscow juu ya hatari ya kutanuka kwa mzozo wa Ukraine.