Urusi yaionya Marekani kuachana na mipango yake ya silaha
27 Mei 2023Urusi imeionya Washington na kuongeza kuwa kwa muda mrefu imekuwa ikipeleka silaha kama hizo barani Ulaya.
Biden amesema mapema leo kwamba amechukizwa sana na ripoti kwamba Urusi imeamua kuendelea na mpango wake wa kupeleka silaha hizo za nyuklia za kimkakati nchini Belarus, baada ya wizara ya mambo ya nje kuulaani mpango huo.
Urusi imesema wana haki na uhuru wa kuhakikisha usalama kwa namna wanayoona inafaa katikati ya vita vilivyoanzishwa na Washington dhidi yao na kuongeza kuwa hatua wanazozichukua zinaendana na wajibu na sheria za kimataifa.
Marekani imesema dunia inakabiliwa na kitisho kikubwa kabisa cha kinyuklia, tangu kile cha Cuba cha mwaka 1962 kutokana na matamshi ya rais Vladimir Putin juu ya mzozo wa Ukraine, lakini Moscow inasema msimamo wake umetafsiriwa vibaya.
Soma Zaidi: Belarus yasema shinikizo la Magharibi limefanya ipokee silaha za nyuklia