1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yabadilishana wafungwa na mataifa ya Magharibi

2 Agosti 2024

Urusi imekamilisha mpango kabambe wa kubadilishana wafungwa na Marekani pamoja na mataifa mengine ya Magharibi.

https://p.dw.com/p/4j22f
Urusi | Gereza la Lefortovo huko Moscow
Waya yenye miiba katika ukuta wa gereza la Lefortovo huko Moscow. Gereza la Lefortovo kwa sasa liko chini ya mamlaka ya Wizara ya Sheria ya Urusi.Picha: Vlad Karkov/IMAGO/ZUMA Wire

Mpango huo unafuatia miezi kadhaa ya mazungumzo ya siri, na hatimaye kumalizika kwa mabadilishano ya wafungwa katika uwanja wa ndege wa mji mkuu wa Uturuki, Ankara. Ujerumani imechangia pakubwa kuwezesha ufanikishaji wa zoezi hilo, ambapo Moscow imewaachilia wafungwa 16 huku raia wa Urusi wanane waliokuwa wakizuiliwa Magharibi wakiachiliwa pia. Mwandishi wa habari wa Marekani Evan Gerhkovich na kanali wa idara ya Ujasusi wa Urusi Vadim Krasikov ni miongoni mwa watu  26 walioachiliwa kutoka kila upande wakiwemo watoto wawili. Viongozi wa Marekani na Umoja wa Ulaya wamepongeza hatua hiyo.