SiasaUrusi
Urusi yaonya kusambaratika kwa mpango wa usafirishaji nafaka
7 Aprili 2023Matangazo
Onyo la Lavrov linajiri baada ya Rais wa Urusi Vladimir Putin, kusema mwezi uliopita kwamba Moscow inaweza kusitisha ushiriki wake katika mpango huo ikiwa masharti yake hayatozingatiwa.
Mkataba wa usafirishaji nafaka katika Bahari Nyeusi ulisimamiwa na Umoja wa Mataifa na Uturuki ili kupunguza mzozo wa chakula duniani kufuati uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.
Soma pia: Mpango wa usafirishaji nafaka za Ukraine waongezewa muda
Urusi na Ukraine ni wazalishaji wakuu wa bidhaa za kilimo duniani, ikiwa ni pamoja na ngano, shayiri, mahindi na mafuta ya alizeti. Urusi inaongoza pia kwenye soko la mbolea.