Moldova yafanya uchaguzi wa serikali za mitaa
6 Novemba 2023Raia wa Moldova wamewachagua mameya wa vijiji, miji na miji mikuu jana Jumapili baada ya rais wa nchi hiyo Maia Sandu anayeegemea Ulaya kuituhumu Urusi kwa kuingilia uchaguzi huo katika taifa jirani yake wa upande wa magharibi.
Sandu ameituhumu Urusi kwa kununua wapigaji kura na kwa kuhamisha dola bilioni tano kwa makundi ya wahalifu yanayoongozwa na mfanyabiashara mtoro Ilan Shor, ambaye amehukumiwa bila kuwa mahakamani kwa ulaghai.
Uchaguzi wa jana nchini Moldova kuwachagua maafisa 12,000 ulivishirikisha vyama kadhaa kikiwemo chama tawala Party of Action and Solidarity PAS cha rais Sandu na chama cha Chance kinachoegemea Urusi kinashohusiwha na mfanyabiashara Shor.
Chama hiki kilipigwa marufuku Ijumaa iliyopita kisishiriki uchaguzi huo. Huu ni uchaguzi wa mwisho wa kitaifa kabla uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika mwezi Novemba mwaka ujao.
(reuters)