1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Urusi yavurumisha wimbi la mashambulizi kuelekea Ukraine

16 Januari 2025

Urusi imevurumisha wimbi la makombora yapatayo 43 na droni 74 na kuilenga miundombinu ya nishati ya Ukraine hasa katika eneo la magharibi.

https://p.dw.com/p/4pBeJ
Mashambulizi ya Urusi huko Ukraine
Mashambulizi ya Urusi huko UkrainePicha: Anton Shtuka/AP/dpa/picture alliance

Jeshi la Ukraine limesema limefanikiwa kudungua makombora kadhaa. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amelaani mashambulizi hayo huku akiwataka washirika wake kutoa msaada zaidi wa usalama ili kukabiliana na Urusi.

Soma pia: Mashambulizi ya makombora na droni kutoka Urusi yaitikisa Ukraine

Zelensky amezitaka nchi za Magharibi kutumia karibu dola bilioni 250 za mali ya Urusi ambazo zimezuiliwa ili kununua silaha na kuipatia nchi yake. Mashambulizi hayo yanajiri siku moja baada ya Kiev kusema kuwa imefanya shambulio lake kubwa zaidi la anga dhidi miundombinu ya kijeshi ya Urusi.