1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yayadunguwa makombora sita ya Marekani kutoka Ukraine

Hawa Bihoga
30 Aprili 2024

Urusi imesema kuwa imeyadungua makombora sita yaliyotolewa na Marekani kwa Ukraine, huku maafisa katika Rasi ya Crimea wakisema makombora mengine yalidunguliwa kwenye Rasi ya Bahari Nyeusi.

https://p.dw.com/p/4fMnu
Ukraine, Kharkiv
Athari ya mashambulizi ya Urusi katika jimbo la Kharkiv, kaskazini mashariki mwa Ukraine.Picha: Sergey Bobok/AFP/Getty Images

Wizara ya Ulinzi ya Urusi ilisema kwamba iliyaharibu makombora sita katika muda wa masaa 24 yaliyopita bila kutoa maelezo zaidi, huku maafisa katika eneo la Crimea wakiwaonya raia kutookota mabaki yoyote ya aina hiyo ya silaha na badala yake kupiga simu za dharura au polisi.

Soma zaidi: Ukraine: Hali ni mbaya katika mstari wa mbele wa vita

Marekani ilisema ilitoa silaha hizo kwa Ukraine ambayo kwa miezi kadhaa sasa imekuwa ikiomba silaha zenye nguvu zaidi, huku kwenye uwanja wa mapambano ikivizuia vikosi vya Urusi kusonga mbele zaidi.

Kwa sasa, Ukraine inasubiri kuwasili kwa silaha mpya za Marekani, baada ya kuidhinishwa na Rais Joe Biden kufuatia mkwamo wa miezi kadhaa na mabishano makali katika bunge la Congress.