Uturuki inapanga kurefusha mpango wa usafirishaji nafaka
5 Machi 2023Matangazo
Mpango huo wa kusafirisha nafaka kupitia bahari nyeusi uliosimamiwa na Umoja wa Mataifa pamoja na Uturuki, uliokubaliwa mwezi Julai mwaka uliopita, uliruhusu nafaka hizo kusafirshwa kutoka bandari tatu kubwa za Ukraine.
Mpango huo ulirefushwa mwezi Novemba na sasa muda wake unakaribia kumalizika tarehe 18 mwezi Machi.
Umoja wa Ulaya watangaza makubaliano ya kuistaki Urusi kwa uhalifu wa kivita
Waziri Cavusoglu amesema amezungumza na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kuhusu juhudi za kurefushwa kwa mpango huo.
Wiki iliyopita Urusi ilisema itakubali hilo ikiwa maslahi ya watengenezaji wake wa bidhaa za kilimo yatazingatiwa.