Vikosi vya Ukraine vyafanya operesheni 'iliyofaulu' Dnipro
17 Novemba 2023Kupitia taarifa waliyochapisha kwenye mtandao wa kijamii wanajeshi hao wa majini wameongeza kuwa vikosi vyao "vimefanikiwa kupiga hatua mbele katika maeneo kadhaa.
Mapema wiki hii, Andriy Yermak, mkuu wa ofisi ya rais wa Ukraine, alisema wanajeshi wa Ukraine wanafanya kazi ya "kuwaondoa wanajeshi wa Urusi na zana za kivita" katika rasi ya Crimea na wameshafanikiwa ukubwa wa asilimia 70 katika rasi hiyo.
Zelensky: Usambazaji wa silaha Ukraine umepungua kutokana na vita vya Israel na Hamas
Mafanikio ya vikosi vya Ukraine katika eneo la Kherson yanakuja baada ya miezi kadhaa ya operesheni ya kuvikabili vikosi vya Urusi kusini mashariki na mashariki ya nchi hiyo.
Vikosi vya Ukraine vinasema kuwa vilifanya oparesheni 'zilizofaulu' kwenye ukingo wa mashariki wa Dnipro.