1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vikosi vya UN haviondoki!,asema Ban Ki Moon.

Thelma Mwadzaya19 Desemba 2010

Wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wataendelea kuyatimiza majukumu yao nchini Ivory Coast hata baada ya rais anayewania muhula mwengine Laurent Gbabgo kutoa wito wa kuwataka waondoke nchini humo.

https://p.dw.com/p/Qfkl
Vikosi vya UN mjini Abidjan, Ivory CoastPicha: picture alliance / dpa

Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon,ujumbe wa UNOCI ulioko nchini humo, utaendelea kutimiza wajibu wake nchini Cote d'Ivoire kwa minajili ya kuzuwia vitendo vyovyote vinavyochochea ghasia,chuki au mashambulio dhidi ya wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa.Mapema hapo jana Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon alimtolea wito Laurent Gbagbo kuachia ngazi na kumpa nafasi mpinzani wake mkuu.

NO-Flash Demonstrationen in Abidjan Elfenbeiküste
Wafuasi wa Alassane Ouattara:ghasia zimeigubika Ivory Coast kufuatia uchaguzi uliozua utataPicha: Picture-Alliance/dpa

Kauli hizo zimetolewa baada ya Laurent Gbagbo kuwataka wanajeshi hao kuondoka nchini humo kwa madai kwamba wanawaunga mkono waasi ambao ni wafuasi wa Alassane Ouatarra.Umoja wa Mataifa,Marekani,Umoja wa Ulaya pamoja na nchi jirani ya Ivory Coast wamemtolea wito Laurent Gbagbo kuachia madaraka kwa sababu anaendelea kunga'nga'nia ushindi kufuatia duru ya pili ya uchaguzi wa rais iliyozua utata.