Viongozi wa Baraza la Haki la Ulaya waungana dhidi ya Urusi
16 Mei 2023Mkutano huo unajiri mwaka mmoja baada ya Urusi kuondolewa katika Baraza hilo lenye dhima ya kutetea haki za binadamu, demokrasia na utawala wa sheria barani Ulaya.
Kuimarisha hatua za kuiwajibisha Urusi kisheria kwa vifo na uharibifu ambavyo imesababisha nchini Ukraine, ndizo mada zitakazogubika mkutano huo wa kilele huko Reykjavik, ambao ni mkutano wa nne pekee kufanyika katika historia ya miongo saba ya baraza hilo.
Zelenskiy aishukuru Ujerumani, Ufaransa na Uingereza
Hadi kufikia jana jioni, hakukuwa na taarifa rasmi iwapo Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky atashiriki katika mkutano huo.
Zelensky amefanya ziara katika miji mikuu kadhaa ya Ulaya, huku Ujerumani, Ufaransa na Uingereza zikiahidi kuongeza msaada wa silaha kwa Kyiv ambayo katika wiki zijazo inatarajia kufanya mashambulizi dhidi ya vikosi vya Urusi mashariki mwa Ukraine.