Viongozi wa EU wakutana kujadili matokeo ya uchaguzi
17 Juni 2024Matangazo
Uchaguzi wa bunge la Ulaya uliofanyika tarehe 6 hadi 9 mwezi huu wa sita ulivipa mafanikio vyama vya siasa kali vya mrengo wa kulia na kuvishangaza vyama vya siasa za wastaninchini Ujerumani na Ufaransa. Hii inamaanisha nguvu ya Ujerumani na Ufaransa inayochangia pakubwa siasa ya Ulaya kidogo imedhoofika.
Soma pia:Ulaya inajigamba kudhibiti uingiliaji kwenye uchaguzi wake
Kulingana na sheria za umoja huo, marais na mawaziri ndio walio na nafasi ya kumchagua rais wa Halmashauri kuu ya Umoja huo atakayehudumu kwa miaka mitano hadi mwaka 2029. Halmashauri hiyo ndio inayoamua kuhusu bajeti ya miaka saba ijayo ya Umoja huo pamoja na sera zake juu ya kila kitu ikiwemo masuala ya mazingira.