1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Vita vya Gaza: Blinken afanya mazungumzo na Netanyahu

12 Oktoba 2023

Wakati mzozo kati ya Israel na Hamas ukiendelea, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amefanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu mjini Tel Aviv.

https://p.dw.com/p/4XT0Y
Israel Antony Blinken und Benjamin Netanjahu
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken (kushoto) akiwa na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu mjini Tel Aviv. (12.10.2023)Picha: Jacquelyn Martin/Pool via REUTERS

Baada ya mazungumzo ya faragha, Blinken na Netanyahu wamehutubia mkutano wa wanahabari. Netanyahu ameisifu ziara ya Blinken na kuitaja kama mfano ulio wazi wa uungwaji mkono usio na shaka wa Marekani kwa Israel.

Netanyahu amesema rais Joe Biden alikuwa sahihi kabisa kwa kuliita shambulio la siku ya Jumamosi la Hamas kuwa ni "uovu". Kama ishara ya kuafiki, viongozi hao wawili walipeana mikono mara tu baada ya kauli hiyo.

Soma pia: Scholz: Ujerumani kupiga marufuku shughuli za Hamas

Blinken kwa upande wake alijinasibu mbele ya waandishi wa habari sio kama kiongozi tu wa serikali, bali pia Myahudi huku akisimulia historia ya familia yake mwenyewe ilivyonusurika na mauaji dhidi ya wayahudi maarufu kama "Holocaust."

Israel Jerusalem | Antony Blinken, US-Außenminister & Benjamin Netanjahu, Ministerpräsident
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken (kushoto) akisalimiana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu huko Jerusalem (30.01.2023)Picha: Ronaldo Schemidt via REUTERS

Aidha Blinken amesema kuwa yeyote anayetaka amani na haki lazima alaani utawala wa kigaidi wa Hamas huku akisisitiza kuwa Israel ina haki ya kujilinda:

"Hamas ina ajenda moja tu. Kuiangamiza Israel na kuwaua Wayahudi. Hakuna nchi inayoweza au ingeweza kuvumilia mauaji ya raia wake au kurejea kwa hali iliyoruhusu hilo kufanyika. Israel ina haki na wajibu wa kujilinda yenyewe, na kuhakikisha hilo halitokei tena."

Jumuiya ya OIC yalaani mashambulizi ya Israel

Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu inayozijumuisha nchi 57 OIC,  imelaani vikali kile ilichokiita "hujuma za kijeshi za Israel zinazoendelea dhidi ya watu wa Palestina huko Gaza", na kusema Israel "inawajibika kikamilifu" kwa athari za kuendelea kwa uchokozi huo."

Jumuiya hiyo ya OIC yenye makao yake makuu mjini Djedah, Saudi Arabia imesema katika taarifa yake kuwa: " Uchokozi huu wa kikatili dhidi ya Watu wa  Palestinani ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa na za kibinadamu na pia ni uhalifu wa kivita." Huku ikisema wanawake na watoto wameuawa na kujeruhiwa, pamoja na uharibifu wa majengo ya raia na maeneo mengine.

Symbolfoto | Organisation für Islamische Zusammenarbeit
Bendera ndogo ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu inayozijumuisha nchi 57 OIC yenye makao yake makuu mjini Djeddah, Saudi Arabia.Picha: Yasser Al-Zayyat/AFP/Getty Images

Shirika la habari la serikali ya Syria SANA limeripoti kuwa rais wa Syria Bashar al-Assad amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na mwenzake wa Iran Ebrahim Raisi na walizungumzia hali ya Ukanda wa Gaza, na kueleza nchi zote mbili zinawaunga mkono watu wa Palestina ambao wamesema "wanafanyiwa uhalifu na wana haki ya kujizatiti ili kutetea haki yao iliyo halali."

Hamas inazingatiwa na  Marekani , Umoja wa Ulaya ikiwemo Ujerumani na baadhi ya mataifa mengine kuwa kundi la kigaidi.

Idadi ya vifo huenda ikaongezeka mno Gaza

Shirika la Umoja wa Mataifa la uratibu wa masuala ya kibinadamu OCHA limeripoti kuwa mashambulizi ya Israel huko Gaza yamesababisha uharibifu wa zaidi ya nyumba 12,600 huku raia wengi eneo hilo wakikabiliwa na hali mbaya mno kutokana na uhaba wa maji safi, mafuta, chakula na dawa.

Israel Angriffe auf Gaza
Njiwa akiruka juu ya vifusi vya nyumba zilizoharibiwa na mashambulio ya Israel huko Khan Younis kusini mwa Ukanda wa Gaza: Oktoba 11, 2023.Picha: Ibraheem Abu Mustafa/REUTERS

OCHA imeendelea kuwa jumla ya hospitali 13 huko Gaza hazina uwezo wa kufanya kazi kwa ukamilifu kutokana na uhaba wa maji na vifaa muhimu vya matibabu, na kwamba zaidi ya watu 650,000 wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa maji.

Soma pia: Ajenda ya mahusiano kati ya Israel na mataifa ya kiarabu

Kuna hatari ya kuongezeka kwa vita hivyo ambavyo vimegharimu maisha ya watu wasiopungua 2,600 kwa pande zote mbili. Kivuko pekee kinachounganisha ukanda Gaza na Misri cha Rafah kilifungwa hapo jana lakini Misri imesisitiza kuwa bado kipo wazi na kinafanya kazi, huku serikali ya Cairo ikiendeleza mazunguzo na Israel na Marekani ili kuruhusu utoaji wa misaada kupitia kivuko hicho kuelekea ukanda wa Gaza.