1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Waasi wa M23 wachukua mji muhimu wa Minova Kongo Mashariki

22 Januari 2025

Kundi la waasi wa M23 limeutwaa mji wa Minova ulioko mashariki, ambao ni njia muhimu ya usambazaji kuelekea mji mkuu wa jimbo la Goma.

https://p.dw.com/p/4pSST
DR Kongo | Waasi wa M23
Waasi wa m23 wamechukuwa maeneo makubwa ya mkoa wa Kivu Kaskazini na sasa wanatishia mji wa Goma.Picha: Moses Sawasawa/AP Photo/picture alliance

Jeshi nchini Jamhuri ya kideomkrasia ya Kongo limekiri kwamba vikosi vya waasi wa M23 vimesonga mbele katika uwanja wa mapambano katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo la Minova ambapo kundi hilo lenye silaha na linalopambana na jeshi la serikali limeteka kitovu cha biashara mjini Goma.

Msemaji wa jeshi la Kongo Sylvain Ekenge amesema katika taarifa kwamba wapiganaji wa M23 wamepiga hatua katika maeneo ya Bweremana huko Kivu Kaskazini na Minova huko Kivu Kusini.

Soma pia: Vita Mashariki mwa Kongo vimeendelea kusababisha umwagaji damu

Kuanguka kwa maeneo hayo hasa Minova kwa wapiganaji wa M23 wanaoungwa mkono na jeshi la Rwanda kunazidi kuudhoofisha mji mkuu wa mkoa Goma katika mzozo ambao umesababisha mamia kwa maelfu ya watu kuyakimbia makazi yao.

Umoja wa Mataifa umesema kwamba zaidi ya watu 230,000 tayari wamekimbia ghasia mashariki mwa DRC tangu Januari mosi mwaka huu.