1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPakistan

Wabunge wa Pakistan wamchagua Shehbaz kuwa Waziri Mkuu

4 Machi 2024

Wabunge wa Pakistan wamemchagua Shehbaz Sharif kuwa waziri mkuu mpya wa nchi hiyo kwa mara ya pili, wiki kadhaa baada ya kufanyika uchaguzi mkuu ambao baadhi ya wanasiasa wamesema ulijaa udanganyifu.

https://p.dw.com/p/4d7rC
Pakistan, Lahore | Shehbaz Sharif
Waziri Mkuu wa Pakistan, Shehbaz Sharif Picha: K.M. Chaudary/AP/picture alliance

Spika wa Bunge la Pakistan , Ayaz Sadiq alitangaza kuwa Sharif alipata kura 201 na kumshinda mwanasiasa wa muungano Sunni Ittehad, Omar Ayub aliyejingia kura 92.

Wakati wa kura hiyo, washirika wa Waziri Mkuu wa zamani aliye gerezani Imrah Khan, walipinga zoezi hilo kwa kupiga kelele ukumbini na pia kutoka tuhuma za kuwepo dosari na vitendo vya udanganyifu katika uchaguzi wa mwezi uliopita.

Sharif ndiye alichukua nafasi ya Khan baada ya kiongozi huyo kuondolewa madarakani kwa kura ya kutokuwa na imani bungeni mnamo Aprili 2022.

Kwenye hotuba yake ya kwanza Shariff alikosoa matendo hayo ya wanasiasa wa upinzani na kuwahimiza kutumia nafasi iliyopo kutafuta maridhiano na kufanya kazi pamoja kwa maslahi ya Pakistan.