1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPanama

Raia wapiga kura katika uchaguzi wa rais nchini Panama

5 Mei 2024

Wananchi wa Panama wameanza hivi leo kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa urais unaowashirikisha wagombea wanane.

https://p.dw.com/p/4fWXb
Panama - Raia wakisubiri kupiga kura katika uchaguzi mkuu
Raia wa Panama karibu milioni tatu waliojiandikisha watamchagua rais, wabunge na viongozi wa serikali za mitaaPicha: Daniel Becerril/REUTERS

Mbali na kumchagua rais, watu karibu milioni tatu waliojiandikisha watawachagua pia wabunge na viongozi wa serikali za mitaa katika nchi hiyo ya Amerika ya Kati.

Wagombea wanaowania urais ni Jose Mulino, Romulu Roux na Ricardo Lombana ingawa hadi sasa Jose Mulino ndiye anayetajwa kuongoza katika kura za maoni kwa takriban asilimia 37.

Rais Laurentino Cortizo wa chama cha mrengo wa kati cha PRD ataondoka madarakani baada ya kumaliza muhula wake uliokumbwa na madai ya kuenea kwa rushwa nakuongezeka kwa viwango vya umasikini.