1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahouthi kuishambulia Israel ikiwa itakiuka makubaliano

17 Januari 2025

Waasi wa Houthi nchini Yemen wametishia kufanya mashambulizi zaidi dhidi ya Israel ikiwa nchi hiyo haitaheshimu makubaliano ya kusitisha mapigano kwa muda wa wiki sita huko Gaza.

https://p.dw.com/p/4pFao
Waasi wa Houthi wa Yemen
Waasi wa Houthi wa YemenPicha: Mohammed Mohammed/Xinhua/picture alliance

Hatika hotuba yake kwenye televisheni jana usiku, kiongozi wa kundi hilo Abdul-Malik al-Houthi amesema mafanikio yaliyofikiwa katika mazungumzo kati ya Israel na Hamas ni "maendeleo muhimu," na kwamba kundi hilo linafuatilia kwa karibu utekelezaji wake.

Soma pia: Israel na Wahouthi washambuliana kwa makombora

Al-Houthi ameongeza kuwa wanamgambo hao wako tayari kutoa msaada wa kijeshi kwa Wapalestina ikiwa kutashuhudiwa ukiukwaji au mashambulizi ya Israel. Waasi wa Kihouthi wamekuwa wakikabiliana na Israel kwa zaidi ya mwaka mmoja ili kudhihirisha uungwaji wao mkono kwa Wapalestina katika vita vya Gaza.