1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wairan wamchagua rais mpya

14 Juni 2013

Wagombea kiti cha rais nchini Iran wamewatolea wito wapiga kura wateremke kwa wingi vituoni katika uchaguzi ambao kambi ya wapenda mageuzi walioungana wanategemea kuibuka na ushindi dhidi ya wahafidhina waliogawanyika.

https://p.dw.com/p/18pEl
Wagombea sita wa kiti cha rais,Said Jalili,Ali Akbar Welayati,Mohammed Bagher Ghalibaf,Mohsen Rezai,Hassan Rohani,Mohammad Gharazi

Wa kwanza aliyeteremka kupiga kura alikuwa kiongozi wa kidini Ali Khamenei aliyewahimiza wapiga kura kwa kusema neema na raha nchini vitategemea chaguo lao kwa mtu anaefaa na kushiriki kwao katika zoezi hilo.

Zaidi ya wapiga kura milioni 50 na laki tano wanatakiwa wateremke viotuoni kumchagua rais mpya atakaeshika nafasi inayoachwa na Mahmoud Ahmadinedjad ambae katiba haimruhusu kupigania mara ya tatu.

Vituo vya uchaguzi vimefunguliwa tangu saa mbili asubuhi saa za Iran ambazo ni sawa na 11 na nusu alfajiri huko Afrika Mashariki na vimepangwa kufungwa saa kumi baadae.Hata hivyo kuna uwezekano zoezi hilo likarefushwa hadi saa tatu na nusu usiku kwa saa za Afrika mashariki.Wairan wanawachagua pia wawakilishi wa mabaraza ya miji.

Chaguo ni kati ya Hassan Rohani,mchamngu mwenye umri wa miaka 64 na mgombea pekee wa kambi ya wapenda mageuzi na wagombea watatu wa kihafidhina:waziri wa zamani wa mambo ya nchi za nje Ali Akbar Welayati,meya wa Teheran Mohammad Bagher Ghalibaf na kiongozi wa tume katika mazungumzo ya kinuklea Said Jalili.

Wagombea wengine wawili Mohsen Rezai na Mohammad Gharazi hawana nafasi yoyote ya kushinda.

""Msifikiri kama hamjenda kupiga kura,matatizo yatafumbuliwa" amesema Hassan Rohani baada ya kupiga kura mjini Teheran.Huu ni mustakbali wa taifa.Mchagueni yule ambae ataweza kukidhi japo kidogo mahitaji ya umma."Amesema mgombea huyo wa kambi ya wapenda mageuzi.

Milolongo ya watu wanasubiri zamu yao

Iran Präsidentschaftswahlen 2013
Wanawake wanapiga kuraPicha: IRNA

Rais wa zamani Akbar Hachémi Rafsandjani anaemuunga mkono Rohani amesema anataraji uchaguzi utasaidia kuimarisha "mshikamano wa kitaifa."

Katika kambi ya wahafidhina,meya wa Teheran Ghalibaf amewatolea wito wagombea wote "waheshimu uamuzi wa wapiga kura".Nae Ali Akbar Welayati amewataka wairan wote wakapige kura akisema "kura yao itamaanisha kuuiunga tena mkono jamhuri ya kiislam."

Vituo vya televisheni vinaonyesha picha za milolongo ya watu wanaopiga foleni kusubiri zamu yao ya kupiga kura katika mitaa kadhaa ya mji mkuu Teheran.

Duru ya pili itaitishwa June 21 ikiwa hakutakuwa na mgombea atakaejingia zaidi ya asili mia 50.1 ya kura.Matokeo ya awali huenda yakaanza kutangazwa kesho.Lakini baraza la walinzi wa katiba,lililopewa jukumu la akusimamia uchaguzi huo limeshasema matokeo yatatangazwa na wizara ya mambo ya ndani na hakuna anaeruhusiwa kujitangaza mshindi kabla ya hapo.

Marekani inashukumu kama mageuzi yatafanyika

Iran Innenansichten eines Gottesstaates
Kiongozi wa kidini Ali KhameneiPicha: Simon Rilling

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa anaeshughulikia masuala ya haki za binaadam nchini Iran,Ahmed Shaheed amesema hali namna ilivyo hairuhusu kuutaja uchaguzi huo kuwa ni huru na wa haki na serikali ya mjini Washington imekosoa "ukosefu wa uwazi " na kuondowa uwezekano wa kufanyika mageuzi katika nchi hiyo.

Mwandishi:Hamiodu Oummilkheir/AFP

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman