Waislamu waghadabishwa na kisa cha kukanyagwa Quran
21 Julai 2023Katika baadhi ya mataifa kulifanyika maandamano baada ya swala ya Ijumaa kuonyesha ghadhabu yao.
Nchini Iran, Iraq na Lebanon, waandamanaji walipanga kuandamana baada ya mhamiaji mmoja kutoka Iraqi anayeishi Sweden kupewa kibali na polisi cha kufanya maandamano na kushuhudiwa akikanyaga nakala ya kitabu cha Quran, nje ya ubalozi wa Iraq.
Soma pia: Iraq yamfukuza Balozi wa Sweden kufuatia kisa cha "kunajisiwa" Quran
Waziri mkuu wa Iraq, Mohammed Shia al-Sudani ameagiza kufukuzwa kwa balozi wa Sweden nchini humo na mwakilishi wao nchini Sweden kurudishwa nyumbani, wakati kundi la wanamgambo wa Shia nchini Lebanon la Hezbollah likiitisha maandamano na kiongozi wake Hassan Nasrallah akiwataka Waislamu kushinikiza serikali zao kuwafukuza mabalozi wa Sweden.