1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiKenya

Wakenya waandamana kupinga ongezeko la kodi

20 Juni 2024

Waandamanaji nchini Kenya wanafanya maandamano mapya kote nchini Alhamisi kupinga mapendekezo ya ongezeko la kodi katika muswada wa sheria ya fedha ambao wengi wanahofia litazidisha gharama za maisha.

https://p.dw.com/p/4hIRi
Maandamano Kenya
Wakenya wanaandamana kupinga ongezeko la kodi katika mswada wa fedhaPicha: Thomas Mukoya/REUTERS

Serikali ya Rais William Ruto inayokabiliwa na uhaba wa fedha ilikubali kufanya mabadiliko baada ya mamia ya waandamanaji vijana kukabiliana na polisi katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi.

Soma pia: Watu 200 wakamatwa maandamano ya ongezeko la kodi Kenya

Hata hivyo, serikali ya Kenya bado inaazimia kuendelea na hatua za kuongeza kodi na inatetea nyongeza zilizopendekezwa ikisema zinahitajika ili kuijaza hazina yake, hatua itakayosaidia kupunguza utegemezi wa kukopa kutoka nje.

Soma pia: Kenya yaondoa tozo kwa mkate kufuatia maandamano

Waandamanaji wameapa kuingia barabarani kote nchini Kenya, ikiwa ni pamoja na katika mji wa bandari wa Mombasa na pia katika mji wa Kisumu ambao ni ngome kuu ya upinzani.