1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPakistan

Wanajeshi sita wa Pakistan wauawa na wanamgambo

Saleh Mwanamilongo
5 Oktoba 2024

Mapigano yametokea katika eneo lenye utulivu la kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo, ambako wanajeshi sita wa Pakistani wameuawa katika mapigano na Wanamgambo wa Kiislamu.

https://p.dw.com/p/4lRL4
Wanajeshi sita wa Pakistan wauawa katika mapigano na wanamgambo wa Kiislamu
Wanajeshi sita wa Pakistan wauawa katika mapigano na wanamgambo wa KiislamuPicha: FAROOQ NAEEM/AFP

 Jeshi limesema katika taarifa hii leo kwamba Luteni Kanali Muhammad Ali Shoukat, ambaye alikuwa akiongoza wanajeshi kukabiliana na wanamgambo, ni miongoni mwa waliouawa, usiku wa kuamkia leo, katika wilaya ya Waziristan Kaskazini, ambayo inapakana na Afghanistan. Eneo linalojulikana kama ngome ya shughuli za wanamgambo wa Kiislamu nchini Pakistan.

Wakati huo huo, Waziri wa mambo ya nje wa India ametangaza kuzuru Pakistan baadaye mwezi huu kuhudhuria mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai. Hiyo ni ziara ya nadra ya afisa wa juu wa India nchini Pakistan.

Subrahmanyam Jaishankar atakuwa waziri wa kwanza wa mambo ya nje wa India kuzuru Pakistan katika kipindi cha takriban muongo mmoja.