1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Wanajeshi wa K. Kaskazini wajiandaa kuingia Ukraine

5 Novemba 2024

Rais Volodymyr Zelenskiy wa Ukraine amedai kuwa wanajeshi 11,000 wa Korea Kaskazini wamewasili katika eneo la mpakani la Urusi la Kursk, huku kukiwa na hofu kwamba watapelekwa katika uwanja wa mapambano nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4mcKH
Ukraine  | Rais Volodymyr Zelenskiy akiwa na maafisa wa kijeshi.
Rais Volodymyr Zelenskiy wa Ukraine akiwa na maafisa wenginePicha: UKRAINIAN PRESIDENTIAL PRESS/REUTERS

"Kulikuwa na ripoti nyengine kutoka kwa shirika letu la kiintelijensia leo kuhusiana na wanajeshi wa Korea Kaskazini nchini Urusi, wanajeshi 11,000 katika eneo la Kursk. Tunaona ongezeko la Wakorea Kaskazini ila kwa bahati mbaya hatuoni ongezeko la jawabu kutoka kwa washirika wetu."

Haijafahamika bado iwapo wanajeshi hao wa Korea Kaskazini watapelekwa kupambana na katika ardhi ya Ukraine au katika maeneo ya Urusi yaliyokaliwa na Ukraine, ambayo yanajumuisha sehemu za mji wa Kursk.

Soma pia:Zelensky asema wanajeshi 11,000 wa Pyongyang wako Kursk

Marekani kupitia wizara yake ya ulinzi inaamini kwamba kuna hadi wanajeshi 12,000 wa Korea Kaskazini nchini Urusi.