Zelensky asema wanajeshi 11,000 wa Pyongyang wako Kursk
5 Novemba 2024Katika hotuba yake ya kila jioni kwa njia ya vidio jana Jumatatu, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, alisema kuwa wanaona ongezeko la idadi ya wanajeshi wa Korea Kaskazini, lakini hawaoni kuongezeka kwa msaada wa silaha kutoka kwa washirika wao.
Zelenskiy: Mataifa ya magharibi mnapaswa kutusaidia zaidi
Zelensky amesema taarifa hiyo inatokana na uchunguzi wa idara ya kijasusi ya nchi hiyo.
Haijabainika ikiwa wanajeshi wa Pyongyang watapigana Ukraine
Ukraine inadhani kuwa hivi karibuni, wanajeshi wa Korea Kaskazini watatumwa na Urusidhidi yake, ingawa wanadiplomasia wa Umoja wa Mataifa pia wamesema wanajeshi hao wanaweza kupelekwa nchini humo labda kutekeleza majukumu ya mipangilio.
Guterres aonya kutumika kwa wanajeshi wa Pyongyang, Ukraine
Bado haijabainika wazi ikiwa wanajeshi wa Korea Kaskazini wanaweza kupelekwa kupigana katika ardhi ya Ukraine ama katika maeneo ya Urusi yanayokaliwa na Ukraine, yanayojumuisha sehemu za Kursk.