1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapalestina 2,200, wakiwemo watoto 724 wameuawa

14 Oktoba 2023

Idadi ya Wapalestina waliouawa katika mashambulizi ya Israel kwenye Ukanda wa Gaza imepanda na kufika 2,200, miongoni mwao wakiwamo watoto 724, hii ikiwa ni kwa mujibu wa wizara ya Afya ya Gaza.

https://p.dw.com/p/4XXEK
Gazastreifen Khan Younis Luftangriff
Picha: Belal Khaled/Anadolu/picture alliance

Aidha, wizara hiyo imeripoti kuwa Wapalestina wengine 8,714 wamejeruhiwa. Wakati huo huo, Umoja wa Mataifa umesema, zaidi ya majengo 1,300 yameharibiwa katika ukanda wa Gaza baada ya wiki moja ya mashambulizi yanayofanywa na jeshi la Israel.

Shirika la masuala ya kiutu la Umoja huo, OCHA limeeleza kuwa makazi  5,540 katika majengo hayo yameharibiwa, na nyumba nyingine 3,750 zimeharibiwa vibaya kiasi kwamba haziwezi kutumika tena kama makazi ya watu.

Soma pia: Maelfu wakimbilia kusini mwa Gaza kukwepa jeshi la Israel

Hayo yanajiri wakati wakaazi takriban milioni 1.1 wa mjini Gaza wameamriwa na Jeshi la Israel kuondoka kwenye maeneo yao upande wa kaskazini na kuelekea upande wa Kusini.

Israel imeanzisha vita dhidi Gaza, baada ya kundi la Hamas linaloudhibiti ukanda huo kufanya mashambulizi ya kushtukiza dhidi ya Israel Jumamosi iliyopita, ambayo yameuwa Waisraeli zaidi ya 1300.

Marekani, Umoja wa Ulaya, Ujerumani ikiwemo, pamoja na nchi nyingine kadhaa, huichukulia Hamas kuwa kundi la kigaidi.