Wapatanishi wapiga hatua katika juhudi za makubaliano Gaza
9 Januari 2025Matangazo
Afisa wa Palestina anayehusika katika mazungumzo hayo, amesema kutokuwepo kwa makubaliano rasmi hadi sasa hakumaanishi kuwa mazungumzo yamefeli na kwamba hizo ni juhudi za dhati za kufikia makubaliano.
Wakati mazungumzo hayo yakiendelea mjini Doha, Qatar, jeshi la Israel limefanya mashambulizi leo katika Ukanda wa Gaza na kusababisha vifo vya Wapalestina 17.
Vifo hivyo vimefikisha idadi jumla ya watu waliouawa kutokana na mashambulizi ya Israel huko Gaza ndani ya saa 24 zilizopita kuwa watu 70.
Qatar, Marekani na Misri zinajitahidi kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano hayo yaliyodumu kwa miezi 15 na kuachiliwa kwa mateka kabla ya Rais Joe Biden hajaondoka madarakani.