1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wataalamu waonya kitisho cha mafuriko nchini Ujerumani

3 Januari 2024

Wataalamu nchini Ujerumani wanahimiza kutathminiwa upya kwa mikakati ya kukabiliana na mafuriko wakati nchi hiyo ikiendelea kukabiliana vikali na mafuriko.

https://p.dw.com/p/4aoz3
Ujerumani | Mafuriko mji wa Verden
Miji kadhaa nchini Ujerumani imekumbwa na mafuriko kutokana na kufurika kwa mito.Picha: Alexander Koerner/Getty Images

Mamlaka ya hali ya hewa imetabiri kuwa mvua zitaendelea kunyesha hadi mwishoni mwa juma, jambo linalozidisha mashaka kwa mamlaka.

Ralf Merz, mtaalam katika Kituo cha Helmholtz cha Utafiti wa Mazingira huko Halle amesema katika kipindi hiki cha mabadiliko ya hali ya hewa, ulimwengu utashuhudia katika siku zijazo aina nyingine za mafuriko.

Mashamba kadhaa katika jimbo la kaskazini la Lower Saxony yamejaa maji, huku kukishuhudiwa mafuriko ya mto Elber. Baadhi ya maeneo ya majimbo ya North Rhine-Westphalia, Saxony-Anhalt na Thuringia pia yameathirika na mafuriko hayo.

Kwa mujibu wa ofisi ya Huduma ya Hali ya Hewa ya Ujerumani (DWD), mvua kubwa inatarajiwa katika majimbo ya Lower Saxony hadi Alhamisi na huko Thuringia hadi siku ya Ijumaa.