Mzozo wa Mashariki mwa Kongo wazidi kuleta wasiwasi
27 Machi 2024Kanyabayonga, Lubero katika Kivu ya Kaskazini, na Minova, katika Kivu ya Kusini, ni kati ya maeneo yenye wakimbizi wengi zaidi, lakini, ni miongoni mwa maeneo yanayosahaulika sana linapokuja suala la msaada wa kibinadamu.
Baadhi ya maeneo ya wakimbizi wa vita hayafikiwi na misaada ya kibinadamu katika mikoa ya Kivu Kaskazini na kivu Kusini kutokana na kuzingirwa.
Soma pia:Takriban raia 11 wameuawa mashariki mwa DR Congo
Msaada wa kibinadamu haufiki kwa watu wenye mahitaji na juhudi za kufikisha msaada wa kibinadamu katika maeneo haya yaliyozingirwa zimekwama.
Wafanyakazi wa kibinadamu wanathibitisha kushindwa kwao kufikia baadhi ya maeneo, siyo kwa sababu ya hofu, bali kwa sababu si rahisi kufikia baadhi ya maeneo ambayo yanadhibitiwa na waasi wakati wote.
Msaidizi wa shughuli za kibinadamu ambaye hakutaka kutajwa jina lake amesema haya alipozungumza na DW "Hali huko Kivu Kaskazini ni ngumu sana kwa sasa. Ni wachache wanaoweza kufikia maeneo fulani ya wakimbizi, kwa upande mmoja, watu wanashindwa kufika na kwa upande mwingine, sehemu kubwa ya Kivu Kaskazini imevamiwa na waasi, ambayo inamaanisha kwamba hatuwezi kufika mara kwa mara."
Wakati huo huo, wakimbizi wa vita walioko katika maeneo yaliyozingirwa zaidi wanakabiliana na mapigano makali. Wakimbizi 12 wamepoteza maisha katika kipindi cha siku 10 tu kutokana na njaa na ukosefu wa huduma za matibabu, kama anavyothibitisha Aimé Mbusa Mukanda, mwanaharakati wa shirika za kiraia
Soma pia:M23 wadhibiti eneo jingine wakati mapigano yakiendelea kwa siku ya tatu Kongo
Zaidi ya wakimbizi 12 wamefariki kwa njaa kutokana na kukosa dawa ndani ya eneo la Kitala na kwenye eneo la Kanyabayonga Rutshuru ambako kuna wakimbizi waliokimbia vita Rutshuru, Kibirizi na Nyanzale.
"Na wakati nilipozungumza na wakubwa wa makambi, wanakiri kwamba serikali ilituma misaada, lakini haukuwafikia vizuri hawa wakimbizi. Na tunahofia kwamba hao wanasiasa wamefanya ubadhirifu kwenye fedha hizo. Na ndio maana tunaomba serikali iongeze nguvu ili kujua hiye fedha imepotelea wapi hasa na akamatwe," amesema Aimé Mbussa Mukanda wa mashirika ya kiraia.
Wakimbizi wa Vita walioko katika maeneo yanayofikiwa na misaada michache ya kibinadamu bado wanakabiliwa na hatari kubwa ya kifo, ambayo inaelekea kwenye janga la kibinadamu, ikiwa serikali haitachukua hatua muhimu na serikali ya Kongo pamoja na Jumuiya ya kimataifa.
Soma pia:Mukwege aonya kuhusu kuondoka haraka jeshi la MONUSCO