1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiZambia

Watu 10 wafariki dunia baada ya mgodi kuporomoka Zambia

8 Oktoba 2024

Takriban watu 10 wamekufa na idadi ya wengine isiyojulikana hawajulikani walipo baada ya mgodi kuporomoka katikati mwa Zambia.

https://p.dw.com/p/4lWGB
Tanzania | Nyarugusu |Geita
Wachimbaji madini wa Tanzania wakitafuta dhahabu kwenye mgodi ulioko Nyarugusu, Mkoa wa Geita.Picha: LUIS TATO/AFP

Mamlaka nchini Zambia imesema shughuli ya uokoaji inaendelea japo haijabainika idadi kamili ya wachimbaji madini waliofukiwa chini ya ardhi.

Mgodi huo uliporomoka katika wilaya ya Mumbwa, takriban kilomita 150 magharibi mwa mji mkuu Lusaka. Hata hivyo chanzo cha kuporomoka kwa mgodi huo bado hakijajulikana.

Soma pia:  Mchimbaji apatikana hai wiki nzima baada ya kufukiwa mgodini

Kamishna wa polisi Charity Chanda amesema miili tisa imepatikana kutoka eneo la tukio huku mtu mwengine akifariki dunia wakati akipokea matibabu hospitali.

Mbunge wa eneo hilo Collins Nzovu amefahamisha kuwa wachimba migodi 20 hawajulikani walipo na wanahofiwa wamepoteza Maisha, ingawa polisi haijathibitisha idadi hiyo.