1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUganda

Watu 11 wafariki Uganda baada ya lori la mafuta kulipuka

23 Oktoba 2024

Watu 11 wakiwemo watoto wawili wamekufa nchini Uganda, baada ya lori la mafuta kupata ajali na kulipuka.

https://p.dw.com/p/4m74W
Lori la mafuta nchini Uganda
Lori la mafuta nchini UgandaPicha: Hajarah Nalwadda/AP Photo/picture alliance

Polisi wamesema ajali hiyo ilitokea mida ya saa tisa alasiri katika mji wa Kigogwa, takriban kilometa 25 kaskazini mwa mji mkuu Kampala.

Taarifa ya Polisi imeongeza kuwa baadhi ya miili iliharibiwa na moto kiasi cha kutotambulika huku majengo manne yakiteketezwa pia na moto huo. Lori hiyo ililikuwa ikisafiri kutoka Kampala kwenda Gulu kaskazini mwa Uganda, ambayo ni safari ya takriban kilomita 650.

Katika miaka ya hivi karibuni, Uganda imeshuhudia matukio kadhaa kama hayo ambapo watu hukimbilia kuchota mafuta kutoka kwa lori zilizopata ajali. Haya yanajiri wakati mnamo Oktoba 15,  lori la mafuta liliripuka kaskazini mwa Nigeria   na kuua zaidi ya watu 170.