1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiBurkina Faso

Watu 15 wauawa katika shambulio dhidi ya kanisa Burkina Faso

26 Februari 2024

Takriban watu 15 wameuawa na wengine wawili wamejeruhiwa kufuatia shambulio lililofanywa na watu wenye silaha katika kanisa wakati wa misa ya Jumapili kaskazini mashariki mwa Burkina Faso.

https://p.dw.com/p/4csE3
Wapiganaji wa itikadi kali wakishikilia bunduki karibu na uwanja wa ndege wa Gao
Wapiganaji wa itikadi kali wakishikilia bunduki karibu na uwanja wa ndege wa GaoPicha: ROMARIC OLLO HIEN/AFP/GettyImages

Afisa mmoja wa kanisa, Jean-Pierre Sawadogo ameliambia shirika la habari la AFP kuwa, kanisa katoliki katika kijiji cha Essakane lilishambuliwa.

Sawadogo amedai kuwa, wapiganaji wenye itikadi kali za kidini ndio waliohusika. Hata hivyo hakukuwa na tamko lolote kutoka kwa mamlaka kuhusu shambulio hilo.

Shambulio hilo ni moja kati ya hujuma zinazodaiwa kufanywa na makundi ya watu wenye silaha katika eneo hilo, na ambao wamekuwa wakilenga makanisa na kuwateka nyara viongozi wa kidini.

Kijiji cha Essakane, kiko katika eneo linalojulikana kama "mipaka mitatu" kaskazini mashariki, karibu na mipaka ya Burkina Faso, Mali na Niger.