1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 15 wauwawa Ukanda wa Gaza

Admin.WagnerD22 Agosti 2014

Hali bado imeendelea kuwa mbaya Ukanda wa Gaza. Taarifa kutoka huko zinaeleza watu 15 wamuwawa katika matukio mawili tofauti.

https://p.dw.com/p/1CzB6
Raketenangriff auf Gaza Israel 20.08.2014
Moshi katika Ukanda wa Gaza, mashahidi wakisema unatokana na mashambulizi wa IsraelPicha: Reuters

Idadi hiyo inajumuisha wanaosadikiwa kuwa ni majasusi wa Israel 11 waliouliwa na wanamgambo wa Hamas na Wapalestina wanne waliuwawa kutokana na mashambulizi ya angani ya Israel.

Mauwaji ya watu hao 11 yanafanyika ikiwa siku moja Israel kuwauwa makamanda watatu wa Hamas kwa mashambilizi yake angani kwenye nyumba moja huko kusini mwa Ukanda wa Gaza. Hamas iliapa kulipiza kisasi kwa kulengwa viongozi wake. Afisa Usalama alisema watu hao waliuliwa jana mapema katika makao makuu ya polisi ya Gaza. Lakini pia awali walikuwa wamehukumiwa kifungo na mahakama ya Gaza.

Mtoa taarifa alizungumza kwa masharti ya kutotaja jina lake, kwa kuwa hakuwa na mamlaka ya kutoa kuzunguza na waandishi wa habari. Mauwaji hayo vilevile yameripotiwa na mitandao ya Al Rai na Al Majd, ambayo inaunganishwa na kundi la Hamas.

Gazastreifen / Beerdigung der Ehefrau von Hamas-Militärchef Deif
mazishi ya kiongozi wa kijeshi wa Hamas, Mohammed Hamas DeifPicha: Reuters

Kutawanywa kwa maiti mitaani

Shirika moja la habari mjini Gaza liitwalo Maan limesema baadhi ya maiti za waliouwawa zimetupwa katika eneo la chuo kikuuu cha Al-Azhar, tukio hilo linafanyika wakati Israel ikiendelea na kufanya mahambulizi yake ya angani dhidi ya Ukanda wa Gaza usiku wa kuamlia leo huku kwa upande mwingine wanamgambo wakiendelea kuvurumisha makombora katika ardhi ya Israel.

Katika matukio ya hivi karibuni mashambulizi ya Israel yamesababisha vifo vya watu wanne. Kitengo cha dharura mjini Gaza kimesema shambulio moja lililolenga nyumba kwenye eneo la Nusserat limeuwa wanaume wawili wenye umri wa miaka 24 na 22. Watu wengine wawili ambao wameuwawa katika shambulizi la Deir al-Balah, bado hawajaweza kutambuliwa.

Um Mohammed ni mkazi wa mji wa Gaza, analezea masikitika yake baada ya nyumba yao kuteketezwa kabisa na makombora ya Israel. "Hakukua na wapiganaji wa Hamas katika nyumba yatu, tumeijenga hii miaka miwili iliyopita. Mungu anajua namna ilivyokuwa vigumu kuijenga, tuna eneo dogo la ardhi. Tumeishi hapa kwa miaka miwili tu. Mungu atatusaidia":

Kwa hesabu za jumla, wiki sita za mashambulizi ya Israel katika eneo la Ukanda wa Gaza yamesababisha vifo vya Wapalestina 2,083, wengi wa hao wakiwa ni raia, na majeruhi 10,482. Kwa upande wa watoa tiba wanasema miongoni mwa vifo hivyo watoto 561. Lakini Israel kutajawa kuuwawa watu 67 wengi wao wakiwa wanajeshi.

Umoja wa mataifa umerejea tena wito wake wa kuzitaka pande zote hasimu kuacha mapigano, ingawa hadi sasa hakuna ishara yoyote ya pande hizo kurejea katika meza ya majadiliano.

Katika hatua nyingine duru za kidiplomasia zinasema Ujerumani, Ufaransa na Uingereza imewasilisha rasimu ya azimio kwa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lenye kutoa wito wa kutaka kuwepo mpango wa uangalizi wa Umoja wa Mataifa Ukanda wa Gaza na kufungua vizuizi vyote vya ukanda huo.

Mwandishi: Sudi MnetteAFP/DPA/APE
Mhariri: Saumu Mwasimba