1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UgaidiNigeria

Watu 17 wauawa Nigeria kufuatia shambulio la kigaidi

1 Novemba 2023

Watu 17 wamekufa na wengine watano wamejeruhiwa kufuatia shambulio la kigaidi katika kijiji cha Kayayya katika Jimbo la Yobe takriban kilometa 150 kutoka Damaturu, kaskazini mashariki mwa Nigeria.

https://p.dw.com/p/4YGfE
Nigeria Region Borno Boko Haram
Gari ya kundi la kigaidi la Afrika Magharibi ISWAPPicha: Audu Ali Marte/AFP/Getty Images

Shambulio hilo liliendeshwa na wapiganaji wa kundi la ISWAP lenye mafungamano na kundi la kigaidi linalojiita Dola la Kiislamu IS baada ya wanakijiji kukataa kulipa "kodi ya mifugo" kwa kundi hilo.

Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, makundi ya kigaidi yamefanya mashambulizi na utekaji nyara nje ya ngome yao kaskazini mashariki mwa jimbo la Borno na kuvilenga vijiji, kambi za jeshi, shule na masoko.

Soma zaidi:Shambulizi la kigaidi laua wanajeshi 29 Niger

Makabiliano na makundi hayo yamesababisha tangu mwaka 2009 vifo vya takriban watu 40,000 huku wengine karibu milioni mbili wakiyahama makazi yao.