1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 90 wafa maji Msumbiji

8 Aprili 2024

Zaidi ya watu 90 wamefariki dunia baada ya boti yao kupinduka kaskazini mwa Msumbiji siku ya Jumapili (Aprili 7).

https://p.dw.com/p/4eWWL
Wavuvi na mashua zao kaskazini mwa Msumbiji.
Wavuvi na mashua zao kaskazini mwa Msumbiji.Picha: Ariadne Van Zandbergen/africamediaonline/picture alliance

Mamlaka nchini humo zilisema wasafiri hao walikuwa wakikimbia mripuko wa ugonjwa wa kipindupindu na walikuwa wakitoka Lunga kuelekea Kisiwa cha Msumbiji, kando kidogo ya pwani ya Nampula.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya huko, mashua hiyo ilikuwa na uwezo wa kuchukuwa watu 100, lakini wakati inazama ilikuwa imepakia watu wapatao 130.

Soma zaidi: Mapigano mapya Msumbiji yasababisha maelfu kuyakimbia makaazi yao

Shirika la habari la AIM liliripoti kuwa chombo hicho kilipigwa na dharuba kali wakati kikiwa katikati ya mkondo.

Msumbijiinakabiliwa hivi sasa na mripuko mkubwa kabisa wa kipindupindu, ambao haujawahi kushuhudiwa kwa zaidi ya robo karne, kwa mujibu wa Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF).

Tangu mripuko huo uanze mwezi Septemba 2022, zaidi ya watu 37,000 wameshaambukizwa.