Watu wanne wauwawa Isreal
13 Oktoba 2015Kwa mujibu wa jeshi la polisi mtu mmoja ameuwawa na wengine 16 kujeruhiwa katika purukushani zilizotokeandani ya basi. Kituo kimoja cha televisheni nchini humo kimeripoti washambuliaji wawili walifyatua risasi na vilevile kumchoma kisu abiria.
Msemaji wa polisi Micky Rosefeld amesema washambuliaji hao vilevile waliuwawa kwa kupigwa risasi na polisi. Katika eneo lingine la Jerusalem mtu aliyeegesha gari lake katika kituo cha basi, alitoka ghafla na kuanza kuwashambulia waliokuwa kituoni hapo wakusubiri basi kwa kisu.
Vifo vya Tel Aviv
Kwa mujibu wa kituo hicho cha televisheni katika mkasa huo raia mmoja wa Israel aliuwawa na wengine wawili na wengine wawili waliuwawa. Katika mji mwingine uitwao Ra'anana, ulio katika jiji la Tel Aviv, watu wawili watu waili wamekumbwa na mikasa ya kuchomwa visu katika maeneo mawili tofauti.
Msemaji wa pilisi Rosenfeld amesema kipindi kifupi kilichopita raia wa Palestina katika eneo hilo hilo la Ra'anana alijeruhiwa vibaya kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali au risasi baada ya kumchoma kisu mwanamke mmoja wa kiarabu, ambae alikuwa akilia kwa sauti kubwa huku akitaja maneno ya "Mungu Mkubwa".
Kwa Jumatatu pekee watu wanne walijeruhiwa kwa kuchomwa vifu mjini Jerusalem. Waisrael wanne wameuwawa wameuwawa na wengine wengi kujeruhiwa kufuatia kuzuka kwa wimbi la washambuliaji wa Kipalestina wa kutumia visu.
mauji ya watu 16 Ukingo wa Magharibi
Wapalestina 16 kutoka Ukingo wa Magharibi na Jerusalem wameuwawa, lakini zaidi ya nusu ya washambuliji waliuwawa baada ya kutimiza lengo au katika prukushani za mashambulizi.
Wengine waliuwawa na kwa kushambiliwa na vikosi vya usalama vya Israel walikuwa na silaha za moto, mabomu ya machozi katika jitiahada za kusambaraitisha waandamanaji walikuwa wakifnaya mashambilizi kwa kutumia mawe, mabomu ya petroli dhidi ya wanajeshi na raia wengine walikuwa katika vyombo vya usafiri.
Katika Ukanda wa Gaza, Wapalestina 11 waliuwawa wakati walipokuwa wakifanya mashambulizi katika eneo la uzio la mpaka na Israel. Vifo vilitokana na maroketi ya Israel, ikiwa mashambilizi ya kulipiza kisasi dhidi ya mashambilizi mengine ya maroketi yaliofanywa na Wapalestina.
Vurugu hizi za sasa zinatokea miezi 18 baada ya kuvurugika kwa mazungumzo ya amani ya pande hizo hasimu, na Waislamu wa Israel wakiwa na hofu serikali kuwa na mpango wa kubadili hali iliyopo sasa katika eneo takatatifu la Jerusalem.
Mwandishi: Sudi Mnette DPAE
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman