1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Watu wawili wafariki baada ya shambulio mjini Zaporizhzhia

10 Agosti 2023

Maafisa wa Ukraine wamesema hapo jana kuwa watu wawili wamefariki dunia na majengo kadhaa kuharibiwa baada ya shambulio la Urusi katika mji wa Zaporizhzhia kusini mashariki mwa Ukraine.

https://p.dw.com/p/4Uzbg
Ukraine-Krieg Saporischschja Raketeneinschläge an Gebäude
Moja kati ya majengo yaliyoharibiwa na mashambulizi ya Urusi mjini ZaporizhzhiaPicha: Zaporizhzhia administration PO/AP/dpa/picture alliance

Urusi kwa upande wake imeripoti mapema leo kutokea kwa moto mkubwa katika eneo la kukarabati magari mjini Domodedevo, nje kidogo ya mji mkuu Moscow na karibu ya mojawapo ya viwanja vikuu vya ndege nchini humo.

Milipuko miwili ilisikika kabla ya kutokea kwa moto huo.

Wakati hayo yakijiri, Marekani imesema itaipatia Ukraine msaada wa kijeshi wenye thamani ya dola milioni 200 ili kuisaidia nchi hiyo kukabiliana na uvamizi wa Urusi.

Msaada huo utajumuisha silaha, risasi, makombora yenye uwezo mkubwa ya HIMARS, mifumo ya ulinzi wa anga ya Patriot.

Ukraine tayari imepokea misaada ya aina hiyo yenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 43 kutoka kwa Marekani.