1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wazambia wapiga kura leo

20 Septemba 2011

Uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na serikali za mitaa unafanyika hii leo (20.09.2011) nchini Zambia, ambapo vituo vya kupigia kura vinaripotiwa kufunguliwa mapema, huku kukiwa na taarifa za kutokea kwa machafuko kidogo.

https://p.dw.com/p/12cgn
Michael Sata, mgombea urais kwa chama cha Patriotic Front, akipiga kura mwaka 2008
Michael Sata, mgombea urais kwa chama cha Patriotic Front, akipiga kura mwaka 2008Picha: picture-alliance/dpa

Rais Rupiah Banda wa chama kinachotawala cha Movement for Multi-Party Democracy anawania muhula mwengine na mpinzani wake mkuu Michael Sata, wa chama cha Patriotic Front, anawania nafasi hii kwa mara ya pili baada ya kushindwa katika uchaguzi uliopita mwaka 2008.

Kwa mujibu wa taarifa za karibuni zaidi ni kuwa kumetokea vurugu kwenye mtaa mkubwa zaidi wa mabanda wa Kanyama mjini Lusaka.

Thelma Mwadazaya amezungumza na wakaazi mbalimbali wa nchini Zambia kupata sura halisi ya mambo yanavyokwenda.

Mahojiano: Thelma Mwadzaya/Wakaazi wa Zambia
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman