1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Bayrou anusurika na kura ya kutokuwa na imani Bungeni

17 Januari 2025

Serikali ya Ufaransa chini ya Waziri Mkuu mpya Francois Bayrou imenusurika Alhamisi jioni na kura ya kutokuwa na imani Bungeni.

https://p.dw.com/p/4pFZU
Waziri Mkuu mpya wa Ufaransa Francois Bayrou
Waziri Mkuu mpya wa Ufaransa Francois BayrouPicha: Thibault Camus/AP Photo/picture alliance

Bayrou amenusurika na kura hiyo baada ya vyama vya mrengo wa kulia na mrengo wa kati kukataa kuunga mkono hoja iliyowasilishwa na chama cha mrengo wa kushoto cha La France Insoumise (LFI).

Chama hicho kinachoongozwa na Jean-Luc Melenchon kiliitisha kura hiyo baada ya Bayrou kupendekeza kuanzishwa tena kwa mazungumzo kuhusu mageuzi ya mfumo wa pensheni yenye lengo la kusaidia kupunguza nakisi iliyokithiri katika bajeti ya mwaka huu.

Ufaransa  ilikabiliwa na mzozo wa kisiasa mwaka jana wakati Macron alipoitisha uchaguzi wa mapema wa Bunge ambao matokeo yake yamesababisha kuwepo mkwamo mkubwa kutokana na kwamba hakuna chama chenye wingi wa kutosha bungeni.