1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi ziarani barani Afrika

4 Juni 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergey Lavrov amefanya ziara nchini Guinea katika ziara yake ya karibuni zaidi huko Afrika Magharibi, eneo lililokumbwa na mapinduzi kadhaa ya kijeshi.

https://p.dw.com/p/4gcj9
Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergey Lavrov
Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergey LavrovPicha: Khalil Hamra/AP Photo/picture alliance

Taarifa ya serikali mjini Conakry imesema Lavrov alikutana hapo jana na waziri wa mambo ya nje wa Guinea Morissanda Kouyaté, na kwamba mkutano huo ulikuwa wa kujadili ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi.

Baadaye Lavrov alisafiri kuelekea Jamhuri ya Kongo ambako amekutana na Rais Denis Sassou N'Guesso katika mji wa Oyo, hii ikiwa ni kulingana na taarifa rasmi kutoka Brazzaville. 

Soma pia:Sergey Lavrov atofautiana na Marekani na Ukraine juu ya mpango wa amani

Haikuwa wazi ni nchi gani nyingine za kiafrika ambazo Lavrov amepanga kuzitembelea wiki hii.