1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiIsrael

Zaidi ya watu 21,320 wamekufa katika ukanda wa Gaza

Hawa Bihoga
28 Desemba 2023

Wizara ya afya katika Ukanda wa Gaza imesema watu wasiopungua 21,320 wameuawa katika eneo hilo la Palestina tangu kuzuka kwa vita na Israel Oktoba 7 mwaka huu.

https://p.dw.com/p/4aff4
Maiti za watu waliouawa katika ukanda wa Gaza
Maiti za watu waliouawa katika ukanda wa GazaPicha: Ahmad Hasaballah/Getty Images

Msemaji wa wizara hiyo ya afya Ashraf Al-Qudra amesema watu wengine 55,603 wamejeruhiwa katika muda wa karibu wiki 12 za mapigano yaliochochewa na shambulizi la Hamas ndani ya Israel.

Qudra amesema watu wasiipungua 210 wameuawa Gaza katika muda wa saa 24 zilizopita, ikiwemo watu familia nzima.

Katika taarifa yake, wizara hiyo imeelezea wasiwasi juu ya kusambaa kwa maradhi miongoni mwa watoto na ukosefu jumla wa maji, chakula na dawa katika Ukanda huo uliozingirwa.

Wakati huo Misri imethibitisha leo kuwa imewasilisha pendekezo la mpango wa kumaliza vita hivyo ambalo linahusisha hatua tatu, zinazomalizika kwa usitishaji mapigano na kusema inasubiri majibu juu ya mpango huo.