Yoon Suk Yeol afikishwa kortini kwa mara ya kwanza
18 Januari 2025Rais wa Korea Kusini aliyetimuliwa madarakani na Bunge, Yoon Suk Yeol mapema leo amewasili kortini kwa mara ya kwanza kwa ajili ya kusikilizwa kwa kesi muhimu ambayo itaamua kama ipo haja ya kuongeza muda wake wa kuzuiliwa huku wapelelezi wakichunguza jaribio lake liloshindwa la kuweka nchi chini ya sheria ya kijeshi.
Iwapo itaidhinishwa, kama inavyotarajiwa, hati mpya inaweza kuongeza muda wa kuzuiliwa kwa Yoon kwa siku 20. Hatua hiyo itawapa nafasi waendesha mashtaka muda wa kurasimisha mashtaka ya uasi, shtaka ambalo linaweza kumfanya Yoon kufungwa jela maisha au kunyongwa ikiwa atapatikana na hatia.
Soma pia: Mahakama ya Korea Kusini yakataa Rais Yoon kuachiwa huru
Wafuasi wa Yoon walikusanyika nje ya mahakama wakati alipokuwa akiwasilishwa na kuzozana na polisi. Rais huyo aliyesimamishwa kazi aliidumbukiza Korea Kusini katika machafuko ya kisiasa mapema mwezi Desemba na tangu wakati huo nchi hiyo imekuwa katika joto kali la kisiasa.