SiasaKorea Kusini
Yoon Suk Yeol agoma tena kuhojiwa na timu ya wachunguzi
20 Januari 2025Matangazo
Mamlaka imesema ulinzi ulikuwa umeimarishwa katika kituo anakozuiliwa Yoon mjini Seoul kabla ya kesi na Mahakama ya Kikatiba ikiwa inashikilia mashtaka ya kesi na kuamua iwapo itamwondoa madarakani kabisa.
Mmoja wa mawakili wa Yoon amesema walipanga kuhudhuria kikao cha kesi ya mashtaka siku ya Jumanne lakini timu ya wachunguzi ilimfuata Yoon hii leo kumhoji kwa nguvu lakini bila mafanikio.
Yoon amekuwa rais wa kwanza wa Korea Kusini aliye madarakani kukamatwa kutokana na tangazo lake la muda mfupi la sheria ya kijeshi mwanzoni mwa mwezi desemba mwaka uliopita.