1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zaidi ya raia 50 wauawa na ADF mashariki mwa DRC

8 Juni 2024

Zaidi ya watu 50 wameuawa wiki hii katika mashambulizi ya waasi wa ADF mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, huku watu wengi wakiendelea kuyahama makazi yao.

https://p.dw.com/p/4gocE
Mashambulizi ya waasi wenye silaha huko Beni mashariki mwa DRC
Mashambulizi ya waasi wenye silaha huko Beni mashariki mwa DRCPicha: Alexis Huguet/AFP/Getty Images

Waasi wa ADF wenye mafungamano na kundi la kigaidi linalojiita Dola la Kiislamu IS, waliwaua watu 13 katika shambulio la Alhamisi wiki hii katika vijiji vitatu huko Beni katika jimbo la Kivu Kaskazini. Hayo yameelezwa na Kinos Katuo, kiongozi wa mashirika ya kiraia katika kitongoji cha Mamove.

Kundi la ADF , ambalo asili yake ni waasi wenye itikadi kali za kiislamu kutoka Uganda, wamekita mizizi kwa karibu miongo mitatu huko mashariki mwa Kongo. Tangu mwaka 2021, majeshi ya Kongo na Uganda yameendesha operesheni za pamoja dhidi ya ADF huko Kivu Kaskazini na Ituri lakini yameshindwa kukomesha mashambulizi dhidi ya raia.