Zelenskiy atoa wito kwa Biden na Xi kushiriki mkutano
26 Mei 2024Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy ametoa wito kwa Marais Joe Biden wa Marekani na mwenzake wa China Xi Jinping kushiriki mkutano ujao wa amani utakaofanyika mwezi Juni huko Uswizi wakati nchi yake inaendelea kukabiliwa na mashambulizi makali ya Urusi.
Katika ujumbe wa video, kiongozi huyo wa Ukraine amesema mkutano huo wa amani utaionyesha dunia ni nani mwenye dhamira ya kweli ya kuvimaliza vita kati ya Ukraine na Urusi.
Soma pia: Mkutano wa G7 wajadili vita vya Ukraine na Gaza
Kauli ya Zelenskiy ameitoa siku mbili tu baada ya vyanzo vya Urusi kuliambia shirika la habari la Reuters kwamba Rais Vladimir Putin alikuwa tayari kusivitisha vita nchini Ukraine chini ya makubaliano yanayolinda maslahi ya nchi yake.
Hata hivyo, Zelenskiy na washirika wake wanasema makubaliano hayo ya kusitisha vita yataisaidia Urusi kujipanga upya.