1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Zelensky alaani shambulizi la Urusi lililowaua watu 16

6 Septemba 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema watu 16 wameuawa katika shambulizi lililofanywa na Urusi hii leo kwenye soko moja katika jimbo la Donesk mashariki mwa taifa hilo.

https://p.dw.com/p/4W1QL
Donetsk
Askari wa Ukraine huko DonetskPicha: Diego Herrera Carcedo/AA/Picture Alliance

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema watu 16 wameuawa katika shambulizi lililofanywa na Urusi hii leo kwenye soko moja katika jimbo la Donesk mashariki mwa taifa hilo.

Taarifa zinasema watu 28 wamejeruhiwa katika shambulizi linalofanywa wakati waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken akiwa ziarani mjini Kyiv.

Zelensky kupitia mtandao wa ujumbe wa Telegram amelaani shambulizi hilo lililowaua watu wasio na hatia na kuandika kwamba uovu huu wa Urusi ni lazima ushindwe haraka iwezekanavyo.Idadi ya waliuwawa kwenye mashambulizi ya Urusi yaongezeka

Kulingana na Zelensky, shambulizi hilo limefanywa karibu na uwanja wa vita, huku waziri wa mambo ya ndani Igor Kylmenko akithibitisha idadi ya majeruhi katika chapisho kwenye mitandao ya kijamii.