Baraza la mawaziri la Israel laidhinisha makubaliano
18 Januari 2025Mawaziri 24 walipigia kura ya kuidhinisha makubaliano hayo huku wanane wakiyapinga. Hii ni baada ya baraza la usalama kuyaidhinisha makubaliano hayo jana Ijumaa.
Katika awamu ya kwanza ya mpango huo, mapigano yatasitishwa Gaza kuanzia kesho mchana na kwa muda wa wiki sita. Hamas itawaachilia mateka 33 wa Israel, huku mamia ya wafungwa wa Kipalestina wakiachiliwa pia huru.
Soma pia: Baraza la usalama Israel laidhinisha makubaliano ya kusitisha vita
Kulingana na taarifa kutoka kwa nchi tatu wapatanishi ambazo ni Qatar, Misri na Marekani, wanajeshi wa Israel watajiondoa katika baadhi ya maeneo ya Gaza na kuruhusu misaada zaidi kuingia katika Ukanda huo, huku mazungumzo yakitarajiwa kuendelea ili kujaribu kufikia mpango wa usitishwaji kamili wa vita.