Papa Francis awasili Mongolia kwa mara ya kwanza
1 Septemba 2023Akiwa njiani kuelekea Mongolia Papa Francis amesema, yalikua ni matarajio yake kulitembelea taifa hilo kubwa kwa eneo la ardhi lakini lenye idadi ndogo ya watu wanaoishi kwa tamaduni zao za tangu jadi. Lakini pia kutembelea maeneo yenye wakatoliki wachache kama Mongolia ni sehemu ya sera yake inayonuwia kuzungumza na watu na kutatua changamoto zinazowakabili.
Papa Francis amesema ziara yake itasaidia kuelewa vizuri ukimya mkubwa uliopo huko na kuelewa maana yake. Si kiakili bali kihisia, Huku akienda mbali zaidi na kusema labda ingetufaa zaidi watu kuusikiliza muziki wa Borodin, ambao ameeleza ungesaidia kueleza kwa upana ukuu wa Mongolia.
Kiongozi huyo wa kanisa Katoliki anatarajiwa kuwahutubia viongozi wa serikali na wanadiplomasia, pia atakutana na jumuiya ya Kikatoliki ambayo inajumuisha mapadri 25 pekee na watawa 33.
Ziara hiyo ya 43 yaPapa Francis katika muongo wake kama mkuu wa Kanisa Katoliki inalenga kuweka mambo wazi ikiwemo kuboresha uhusiano wa Vatican kwa China na Urusi ambazo mpaka sasa bado hazijampa Papa mwaliko wa kuzitembelea.
Kama ilivyo desturi ya Papa hutuma ujumbe wa salamu kwa viongozi wa kila nchi anayopitia, amefanya hivyo kwa China, ambapo katika ujumbe wake kwa rais Xi Jingping alisema anawatakia kila la heri watu wa China na rais wao yuko kwenye maombi yake kwa mustakabali wa ustawi wa taifa hilo.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje ya China Wang Wenbin amesema Beijing iko tayari kuboresha uhusiano na Vatican, na baraka za Papa zimeonyesha urafiki na nia njema, na China iko tayari kuendelea kufanya kazi na upande wa pili. Ambapo amesema yanahitajika mazungumzo yenye kujenga, maelewano, kuaminiana na kuendeleza mchakato wa kuboresha mahusiano kati ya pande hizo mbili.
Safari hiyo pia ni kipimo cha kuimarika kiafya kwa papa ambaye anaendelea kusafiri sehemu mbalimbali, akitumia kiti cha magurudumu kutokana na maumivu ya goti baada ya kufanyiwa upasuaji mwezi Juni.
Kwenye mkutano wake na wawakilishi wa dini, Papa analenga kuimarisha jumuiya ndogo ya Wakatoliki na kukuza mazungumzo baina ya madhehebu ya dini, pamoja na kuzindua kituo cha hisani cha kusaidia wahitaji kitakacho wahudumia wote bila kujali dini zao.
Kabla ya kuhitimisha ziara yake Mongolia Jumatatu ijayo, Papa Fransis ataongoza hafla kadhaa ikiwemo misa takatifu inayotaraji kufanyika siku ya Jumapili na inatazamiwa kuhudhuriwa na mahujaji kutoka maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Urusi, China, Korea Kusini,Thailand, Vietnam, Kazakhstan,