1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Israel itawaachilia zaidi ya wafungwa 1900 wa Kipalestina

18 Januari 2025

Serikali ya Israel imetangaza leo Jumamosi kwamba jumla ya Wapalestina 1,904 wataachiliwa huru kutoka kwenye magereza na kambi za Israel wakati wa usitishaji mapigano uliokubaliwa kati ya Israel na Hamas hapo kesho.

https://p.dw.com/p/4pK2V
Israel  I Baraza
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akiwa na baraza lakePicha: Koby Gideon/AFP

Serikali ya Israel imetangaza leo Jumamosi kwamba jumla ya Wapalestina 1,904 wataachiliwa huru kutoka kwenye magereza na kambi za Israel wakati wa usitishaji mapigano uliokubaliwa kati ya Israel na Hamas hapo kesho.

Kwa upande wake, Hamas itawaachilia mateka 33 kati ya 98 wa Israel, wakati huo mapigano yatasimama kwa muda wa wiki sita kuanzia kesho Jumapili.

Soma zaidi. Baraza la mawaziri la Israel laidhinisha makubaliano ya kusitisha mapigano.

Kwa mujibu wa serikali ya Israel, Wapalestina hao ni pamoja na 1,167 wakaazi wa Ukanda wa Gaza ambao hawakuhusika katika shambulio la Hamas la Oktoba 7, 2023 nchini Israel. Wapalestina wengine 737 walikuwa wamefungwa jela kwa makosa ya kurusha mawe katika eneo la ukingo wa magharibi, kuvuka mpaka uliozuiliwa na kumiliki silaha kinyume cha sheria.

Wakati mpango huo ukikaribia, Israel yenyewe imeendeleza mashambulizi yake huko Gaza. Mapema leo madaktari katika ukanda wa Gaza wamesema watu watano wameuawa katika eneo la Mawasi. Hadi sasa jumla ya watu 119 wameuawa kwenye mashambulio ya Israel tangu kutangazwa kwa makubaliano ya kusimamisha mapigano siku ya Jumatano.