Kwa wajane Afrika, COVID iliiba waume, nyumba, mustakablali
10 Mei 2022Wakati Anayo Mbah alipopata uchungu na mtoto wake wa sita, mumewe alikuwa anapambana na COVID-19 katika hospitali nyingine mjini Umuida, Nigeria. Jonas, dereva kijana wa teksi ya pikipiki, alikuwa amewekewa hewa ya oksijeni baada ya kuanza kukohoa damu.
Jonas hakuweza kukutana na binti yake, Chinaza. Saa kadhaa baada ya kujifungua, shemeji yake Mbah alipiga simu kuwa ameaga dunia. Wafanyakazi katika hospitali ya kusini mashariki mwa Nigeria walimtaka Mbah na mtoto wake mchanga kuondoka. Hakuna mtu aliyekuja kulipa bili yake.
Mbah alianza taratibu za ujane pale nyumbani alipokuwa akiishi na wakwe zake: Kichwa chake kilinyolewa, na alivaa mavazi meupe. Lakini wiki chache tu baada ya kipindi cha maombolezo ambacho kijadi huchukua miezi sita, ndugu wa marehemu mumewe waliacha kutoa chakula, kisha wakamkabili moja kwa moja.
"Waliniambia kuwa ilikuwa bora kwangu kutafuta njia yangu mwenyewe,'' Mbah, ambaye sasa ana umri wa miaka 29, alisema. "Walisema hata ikibidi niende kuolewa tena, nifanye hivyo. Kwamba kadiri ninavyoondoka nyumbani mapema, ndivyo inavyokuwa bora kwangu na kwa watoto wangu.''
Aliondoka kwa miguu kuelekea nyumbani kwa mama yake akiwa na begi la plastiki tu la vitu vya Chinaza na watoto wake wengine. "Niliamua kwamba ningekufa ikiwa nitaendelea kukaa hapa na watoto wangu,'' alisema.
Soma pia: WHO: Maambukizi ya Omicron barani Africa yamepungua
Kotekote barani Afrika, ujane umewakumba kwa muda mrefu idadi kubwa ya wanawake - hasa katika nchi ambazo hazijaendelea sana katika bara hilo ambapo vifaa vya matibabu ni haba. Wajane wengi ni vijana, wakiwa wameolewa na wanaume wanaowapita umri kwa miongo kadhaa. Na katika nchi nyingine, wanaume mara nyingi huwa na zaidi ya mke mmoja, wakiacha wajane kadhaa wanapofariki.
Na sasa, janga la virusi vya corona limesababisha idadi kubwa zaidi ya wajane katika bara hilo, na wanaume wa Kiafrika wana uwezekano mkubwa wa kufa kwa virusi hivyo kuliko wanawake, hali ambayo imezidisha maswala yanayowakabili. Wanawake kama Mbah wanasema janga hili limechukua zaidi ya waume zao: Katika ujane wao, limewagharimu familia kubwa, nyumba zao na mustakabali wao.
Simulizi hii ni sehemu ya mfululizo wa mwaka mzima wa jinsi janga hili linavyowaathiri wanawake barani Afrika, haswa katika mataifa yenye hali duni. Mara tu wanapogeuka wajane, wanawake mara nyingi hutendewa vibaya na kunyang'anywa urithi. Sheria zinakataza wengi wao kupata ardhi au kuwapa sehemu ndogo tu ya utajiri wa wenzi wao, na wajane katika maeneo kama kusini mashariki mwa Nigeria wanakabiliwa na shutuma kuhusiana na vifo vya waume zao wakati wa kipindi cha maombolezo.
Ukosefu wa elimu ya kuwasadia kujikimu kimaisha
Wakwe wanaweza kudai ulezi wa watoto; jadi inasema watoto ni wa baba. Wakwe wengine huwakana watoto na kukataa kusaidia, hata kama wao ndio chanzo pekee cha pesa na chakula cha familia. Na wajane vijana hawana watoto wakubwa wa kuwasaidia katika jamii zenye umaskini uliokithiri na ajira chache kwa wanawake wenye elimu ndogo.
Soma pia: Bara la Afrika laazimia kuagiza dawa ya kutibu COVID-19
Nchini Nigeria, taifa lenye watu wengi zaidi barani Afrika, takriban asilimia 70 ya vifo vilivyothibitishwa vya COVID-19 vimekuwa vya wanaume, kulingana na data iliyofuatiliwa na Mradi wa Ngono, Jinsia na COVID-19. Vile vile, zaidi ya asilimia 70 ya vifo nchini Chad, Malawi, Somalia na Kongo vimekuwa vya wanaume, kulingana na takwimu za mradi huo, ambao ni hifadhidata kubwa zaidi duniani inayofuatilia tofauti za virusi vya corona kati ya wanaume na wanawake. Nchi nyingine huenda zikaonyesha mwelekeo kama huo lakini hazina rasilimali za kukusanya takwimu za kina.
Wataalamu wanasema baadhi ya wajane walioachwa hawana lolote huku wengine wakishinikizwa kuolewa tena na mashemeji au watengwe. Wajane wanaweza kuanza kudhulumiwa na wakwe zao kabla hata waume zao hawajazikwa.
"Wengine wanachukuliwa kama watu waliotengwa, wakituhumiwa kuhusika na kifo cha mume wao,'' alisema Egodi Blessing Igwe, msemaji wa WomenAid Collective, ambayo imesaidia maelfu ya wajane kwa kuwapa huduma za kisheria za bure na usuluhishi wa familia.
Soma pia: Maambukizi ya Omicron Afrika Kusini huenda yamefikia kilele
Baadhi ya wataalam wanasema wajane wanakabiliwa na hali mbaya zaidi nchini Nigeria. Huko, Mbah sasa analea watoto wake bila msaada wa kifedha kutoka kwa wakwe zake, ambao walichukua hata pikipiki ambayo mumewe alikuwa akiendesha kama teksi. Anafanya kazi nne, ikiwa ni pamoja na moja kama msafishaji katika shule ambapo hawezi tena kumudu kupeleka watoto wake.
Mumewe hakuacha wosia, na hajafuatilia kesi ya kisheria dhidi ya wakwe zake. Anaogopa kwamba ingefanya hali yake tu mbaya zaidi, na kupata wakati itakuwa karibu haiwezekani. Kwa baadhi ya wajane wanaofuata njia za kisheria, wosia huokoa siku, alisema Igwe, na shirika la kutetea haki za wanawake.
Nchini Congo, Vanessa Emedy Kamana alikuwa amemjua mumewe kwa muongo mmoja kabla ya kumpendekezea ndoa. Alifanya kazi kwa msomi huyo kama msaidizi binafsi. Wakati urafiki wao ulipogeuka kuwa wa kimapenzi, Godefroid Kamana alikuwa na umri wa miaka 60, na yeye akiwa mama asiye na mwenzi katika miaka yake ya mwisho ya 20.
Soma pia:Viongozi wa Afrika, Ulaya wabishania udhibiti chanjo za COVID-19
Alipofariki, ndugu walikuja kwenye nyumba ya familia ambapo Kamana alikuwa ameanza kipindi chake cha maombolezo. Kwa ujumla, wajane wanatakiwa kukaa katika nyumba zao na wanaweza kupokea wageni. Muda wa maombolezo hutofautiana kulingana na dini na kabila. Kamana, ambaye familia yake ni Waislamu, alipaswa kukaa nyumbani kwa miezi minne na siku 10. Lakini watu wa ukoo wa mume wake hawakungoja muda mrefu hivyo kumlazimisha yeye na mwanawe mchanga watoke barabarani, usiku wa mazishi yake.
"Nilinyang'anywa kila kitu, mali yangu yote,'' alisema. Alihofia familia ya mumewe ingetafuta haki ya kumlea mwanawe, Jamel, ambaye Kamana alimchukua na kumpa jina lake la ukoo. Lakini jamaa hawakufanya hivyo, kwa sababu mvulana huyo mwenye umri wa miaka 6 sasa, hakuwa mtoto wake wa kumzaa. Hata hivyo, walikusanya haraka mali za kifedha za marehemu.
Soma pia: Rais Ramaphosa akutwa na COVID-19
"Sikuwa na habari kwa sababu nilikuwa nyumbani nikililia mume,'' alisema. "Lakini walikuja na kusema: 'Akaunti hizi za benki ni zetu.''
Yeye, mwanawe na paka wao sasa wanaishi katika nyumba ndogo ambayo mama yake aliijenga kwa ajili ya kukodisha. Kamana anauza nguo za mitumba sokoni. Hapo awali alipokea asilimia 40 ya mshahara wa marehemu mumewe, pesa hizo zitaacha kuja kabisa hivi karibuni.
Inatia uchungu, Kamana alisema, wakati ndugu wa marehemu mumewe wanasisitiza kuwa wamepoteza zaidi ya yeye: "Hakuna atakayeweza kuchukua nafasi yake.''
Haki ya urithi Afrika Magharibi
Katika kanda ya Afrika Magharibi, ujane umejaa hasa katika maeneo makubwa ambapo ndoa nyingi ni za wake wengi. Mke wa kwanza au watoto wake kwa kawaida hudai nyumba ya familia na mali za kifedha.
Saliou Diallo, 35, alisema hangeachwa bila chochote baada ya muongo mmoja wa ndoa kama mumewe hangefikiria kuweka nyumba yake chini ya jina lake badala ya lake. Hata baada ya kifo chake, anaishi kwa hofu kwamba watoto wakubwa wa mumewe au jamaa watajaribu kuchukua makao yake madogo viungani mwa mji mkuu wa Guinea, Conakry.
Chini ya sheria ya Guinea, wake wengi wa mwanaume wanagawana asilimia ndogo ya mali yake, na karibu yote, asilimia 87.5, ikienda kwa watoto wake, alisema Yansane Fatou Balde, mtetezi wa haki za wanawake. Wanawake ni nadra sana kugombea urithi wao, kutokana na unyanyapaa na gharama.
Soma pia: Afrika Kusini yazuia matumizi ya chanjo ya Urusi Sputnik V
Mume wa Diallo, El Hadj, 74, alikuwa akimjengea nyumba yeye na binti yao wa miaka 4 alipougua COVID-19. Diallo aliambukizwa, pia _ na aliogopa. Tayari alijua mzigo wa kupoteza mwenzi wake: Akiwa na umri wa miaka 13, alikua mke wa pili, lakini akawa mjane katika miaka yake ya mapema ya 20.
Jaribio lake lililofuata la kuolewa lilizinduliwa wakati mwanamume huyo alipokosa kuwapa watoto wake watatu. Kisha akatambulishwa kwa El Hadj, ambaye tayari alikuwa ameoa wanawake wengi lakini alikuwa tayari kulea watoto watatu wa Diallo kama wake.
Walikaa miaka kumi pamoja kabla ya virusi kugonga El Hadj. Katika mazungumzo yake ya mwisho na mke wake, alilalamika kwamba nyumba yake haikuwa na madirisha bado. Kwamba hakuwa ameishi muda mrefu vya kutosha kujenga kisima ili asilazimike kubeba maji kichwani kila siku. Kwamba jamaa wengine wangejaribu kumfukuza mara tu atakapoondoka.
Wakati wa maombolezo, mke wa kwanza alikataa kutoa pesa kwa Diallo, ambaye hakuweza kuhudhuria mazishi kwa sababu alipimwa na kuambukizwa virusi. Kisha watoto wa mke wa kwanza walikuja nyumbani kwa Diallo na kuchukua gari ambalo alikuwa amempa. Walichukua hati zake zote na vitabu vya hundi.
Soma pia: HRW: Misaada ya Covid-19 Afrika haikuwafikia walengwa
"Walitaka kunifukuza pia," Diallo alisema. "Niliwaambia: 'Acha nimalize maombolezo yangu na nilione kaburi la mume wangu.'" Watoto waliomba karatasi za nyumba ambayo El Hadj alikuwa amemjengea. Alitoa nakala lakini nyaraka halisi alizihifadhi kwa siri.
Familia yake kubwa hatimaye ilisaidia kupata pesa za kuweka madirisha kwenye nyumba yake. Bado, anahisi kutokuwepo kwa mume wake. Kuna umeme, lakini hakuna taa. Kuta zimekamilika lakini hazijapakwa rangi, na ni viti vichache tu vya lawn vya plastiki na friji ndogo vinavyotoa nyumba.
"Nina hakika Mungu atanishangaza. Ninajisalimisha kwake,'' alisema. "Wakati huo huo ninaishi kwa msaada wa wazazi wangu. Wananiunga mkono, na ninashika imani yangu.''
Katika kesi ya Diallo, sheria imelinda nyumba yake. Lakini wapi sheria kushindwa kuwalinda wajane, utatuzi wa migogoro ya kutorithi mara nyingi huja kwa upatanishi wa familia pekee.
Sintoolewa tena
Huko Nigeria, Roseline Ujah, 49, alitumia miongo mitatu akiwa sehemu ya familia kubwa ya mumewe. Alishiriki kazi za nyumbani na chakula pamoja nao, hata kusaidia kuwatunza mama na baba mkwe wake katika miaka yao ya baadaye.
Soma zaidi: Viongozi wa Kiafrika walihutubia Baraza la Umoja wa Mataifa
Lakini alisema kaka ya mumewe alianza kula njama ya kumzuwilia kurithi pamoja na watoto wake saba kabla hata mume wake, Godwin, hawajazikwa. Shemeji yake aliingilia kati na kufanikiwa kuokoa sehemu ndogo ya ardhi ambapo Ujah sasa analima kakaamu, mboga ya mizizi.
Ujah anaachwa kuhangaika kuokoa maisha ya familia yake, akitengeneza mifagio ya kuuza kwenye soko la ndani. Anajua mume wake angekabili familia yake kwa sababu ya kumtendea vibaya. Bila yeye, anageukia imani yake.
"Ninamtazama Mungu, nikimwambia sina mtu mwingine, "alisema. "Yeye ni mume wangu na baba wa watoto wangu na wa familia, na sitaolewa na mwanamume mwingine."