1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiRwanda

Mashtaka ya mshukiwa mauaji ya kimbari Rwanda yaahirishwa

30 Agosti 2023

Hatua ya kumfungulia mashtaka mshukiwa wa mauaji ya kimbari ya Rwanda Fulgence Kayishema katika mahakama ya Umoja wa Mataifa imecheleweshwa leo.

https://p.dw.com/p/4Vm2h
Fulgence Kayishema appears in the Cape Town Magistrates Court
Picha: Nic Bothma/REUTERS

Hii ni baada ya jaji nchini Afrika Kusini alikokamatwa mshukiwa huyo, kuahirisha kikao cha kusikilizwa kwa ombi la kuhamishwa kwa kesi hiyo.

Kayishema anayedaiwa kushiriki mauaji hayo ya mwaka 1994 na kushikiliwa mnamo mwezi Mei huko Cape Town baada ya zaidi ya miaka 20 akiwa ametoroka, hakuwepo mahakamani.

Mahakama hiyo ya Umoja wa Mataifa ilikuwa imetaka kesi ya Kayishema isikilizwe katika tawi lake mjini Arusha, Tanzania.

Soma pia: UN: Mshukiwa wa mauaji ya kimbari asifunguliwe mashtaka

Hata hivyo, utaratibu wa kisheria ambao ni tofauti na kuhamishwa kwa kesi yenyewe ndio ilikuwa chanzo cha mkanganyiko na kesi hiyo kuahirishwa.

Kayishema mwenye umri wa miaka 62, anatuhumiwa kusimamia mauajiya zaidi ya wanaume, wanawake na watoto elfu 2 waliokuwa wamejificha kanisani wakati wa mauaji hayo.