1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkosoaji wa serikali ya Tanzania aachiwa baada ya kutekwa

13 Januari 2025

Mwanaharakati na mkosoaji wa serikali ya Tanzania Maria Sarungi ameachiliwa baada ya "kutekwa nyara" siku ya Jumapili na watu watatu wenye silaha katika mitaa ya mji mkuu wa Kenya Nairobi.

https://p.dw.com/p/4p6ZW
Tanzania | Maria Sarungi Tsehai
Mwanaharakati na mkosoaji wa serikali ya Tanzania Maria SarungiPicha: Imani Nsamila

Mume wa mwanaharakati huyo aliishutumu idara ya ujasusi ya Tanzania kwa kuhusika na tukio hilo.

Taarifa ya kutekwa kwa Maria Sarungi mtetezi wa haki za binadamu ambaye anakosoa utawala wa rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ziliripotiwa na shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International jana mchana.

Soma pia:Mwanaharakati wa Tanzania Maria Sarungi asema yuko salama baada ya kutekwa nyara Nairobi

Baada muda mfupi baada ya kusambaa kwa taarifa hizo, Mwanaharakati huyo alichapisha kwenye mtandao wa kijamii wa X akisema kwamba sasa yuko salama na kuahidi kuuzungumzia mkasa huu hii leo.

Mkasa huo umetokea wakati Tanzania na Kenya zikiwa zinashutumiwa kwa kuwateka nyara wakosoaji.